Klabu ya Chelsea ipo ukingoni kabisa kukamilika usajili wa mshambuliaji, Liam Rory Delap ambaye amekuwa akiwindwa kwa udi na uvumba na Mashetani Wekundu wa Manchester United.
Delap (22) raia wa England ambaye timu yake ya Ipswich Town imeshuka daraja ameichagua Chelsea licha ya kutakiwa na Man United, Everton na baadhi ya timu kutoka Ujerumani na Italia.
Nyota huyo amependekeza kufanya kazi na kocha wake wa zamani Enzo Maresca aliyefanya naye kazi kwenye timu ya vijana (academy) ya Manchester City huku Chelsea ikitarajiwa kuamilisha kifungu cha kuachiwa (release clause) cha pauni milioni 30.