Uongozi wa Simba umewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuwa watulivu kufautia fununu za mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berbane kupelekwa Zanzibar.
Simba itakuwa mwenyeji wa RS Berkane katika mchezo huo utakaopigwa Mei 25 nchini Tanzania, baada ya ule wa kwanza utakaochezwa Mei 17 mjini Berkane, Morocco.
Hata hivyo hadi sasa Serikali na Mamlaka za soka nchini Tanzania haijatoa taarifa zozote za mchezo huo kupelekwa Zanzibar.
Taarifa ya Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii imeeleza: Taarifa rasmi kuhusu Uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025.
ALSO READ | Magori Aomba CAF Ichunguze Swala la Simba Kubadilishiwa Uwanja Fainali ya CAF…