Alichofanya Rais wa RS Berkane ni Uhuni Mtupu, Kwa Mkapa Lazima Tutacheza
Kwa Mkapa hajawahi kutoka mkubwa yoyote, kwa Mkapa kila mtu anajua kuwa Simba anasubiri Fainali tu achukue Kombe. Huyu Berkane amewahi kufa, Al Ahly amewahi kufa, Wydad amewahi kufa kwa kifupi kila Mkubwa wao amekufa kwa Mkapa.
Huyo Muhuni kwenye slide UKIENDA UTAMUONA kuna KUNGUNI wanamsifia sio sababu ya Uhuni na nafasi zake bali wanajua FAOUZ LEKJA ambaye ni Rais wa Shirikisho la Falme za Morocco ndio mwanadamu anayepigana kuhakikisha Simba wanakosa Ubingwa, Nchi inakosa Ubingwa.
Sasa utanielewa, hii vita ni ya wahuni kwa Wahuni, hii vita bado mbichi na mechi bado itapigwa kwa Mkapa, iwe mvua iwe JUA ngoma itapigwa kwa Mkapa……. Hii ndio Moment ya kigezo cha Mvua kitakapokua sio KIGEZO yaani Mvua haitanyesha na ikinyesha itachesha muda wa kushangilia kombe.
Kuweza kufika Fainali ya Vilabu Barani Afrika maana yake na Sisi tumefika LEVO zao za Uhuni, tupo anga moja hivyo hakuna KUPANIKI hadi dakika ya mwisho hii ni VITA ya Kihuni na wahuni wapo kazini. Hii sio Tanzania ya Kifala, hii nchi imetoa mjumbe wa kamati ya Utendaji CAF, Rais wa CECAFA na Tunafuzu MAAFCON…. Sisi pia WAHUNI.
KWA MKAPA WATACHEZA NA WATAKUFA KIHUNI.
NB:Simba na Berkane Simba kubwa, inavutia kwenye macho ya CAF, na ikicheza SUPER CUP kuna faida kubwa zaidi.