Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga SC ametoa tamko mara tu baada ya Simba SC kupata ushindi mkubwa dhidi ya KMC FC. Kwenye kauli yake ya kitaharuki, ameeleza kuwa tofauti ya Yanga na Barcelona ni maeneo tu. Ameeleza kuwa Yanga SC na Barcelona wote wameshona wapinzani wao wa Derby mara 4 mfululizo.
Aidha Simba SC ameshinda mechi nne mfululizo. Mechi za viporo ambazo zilikuwa mezani kwa Kocha Fadlu Davids limefungwa rasmi jana Jumapili kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya Simba SC kukamilisha mechi nne kwa mafanikio makubwa kwa kukusanya pointi zote 12.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo huo wa nne mfululizo ndani ya siku 10. Simba ilikuwa na mechi nyingi mkononi kutokana na kushiriki kwao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hali ambayo iliwafanya kuchelewa kucheza mechi kadhaa za ligi huku mpinzani wao, Yanga, ikiendelea na ratiba ya kawaida ya ligi.
Ushindi huo umeifanya timu hiyo kufikisha pointi 69 baada ya mechi 26, ikibaki nyuma kwa alama moja tu dhidi ya Yanga ambayo nayo imecheza idadi sawa ya mechi.
Hilo lilikuwa bao la tatu anaruhusu Camara katika mechi nne za viporo. Kipa huyo ameruhusu mabao katika mechi tatu dhidi ya Pamba Jiji (5-1), Mashujaa (2-1) na jana dhidi ya KMC. Mechi pekee aliyotoka bila kuruhusu bao ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania.
Hilo lilikuwa bao la 10 kwa Mukwala msimu huu kwenye ligi, likimweka katika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa Simba nyuma ya Charles Jean Ahoua mwenye mabao 15 na Leonel Ateba mwenye mabao 12.