AFCON 2025: Msuva Mchezaji Bora Taifa Stars Vs Uganda

Mshambuliaji wa Taifa Stars Simon Msuva amekuwa mchezaji bora wa mechi ya Tanzania dhidi ya Uganda kwenye fainali za AFCON 2025 zinazoendelea nchini Morocco.
Msuva amefanikiwa kufunga goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 59 katika sare ya 1-1, goli hilo limemfanya Msuva afikie rekodi ya Mrisho Ngassa ya kuwa mfungaji bora wa muda wote Taifa Stars wakiwa na magoli 25.
Msuva pia anandika rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Taifa Stars aliyefunga goli katika AFCON zote tatu alizosiriki, Tanzania ikiwa imeshiriki kwa mara ya nne.
- AFCON 2019 amefunga vs Kenya
- AFCON 2023 amefunga vs Zambia
- AFCON 2025 amefunga vs Uganda
