CAF Watoa Ratiba Kamili ya Mchezo wa Yanga na FC Kablyie
Mchezo wa Mwisho Kundi B Yanga SC dhidi ya FC Kablyie umepangwa kupigwa Siku ya Jumapili Saa Moja usiku katika uwanja wa New Amaan Zanzibar.
Mchezo huo ni muhimu sana Kwa Yanga Sc ili kuweza kufuzu robo Fainali Klabu Bingwa Afrika. Yanga inahitaji ushindi ili kufuzu pia inamuombea Al Ahly ipate ushindi mnono dhidi ya Far Rabat kutoka Morocco.
Yanga Sc Hadi sasa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Far Rabat ikiwa na Alama 5 huku Far Rabat ikishika nafasi ya Pili ikiwa na Alama 8, huku Fc Kablyie yenyewe inashika Mkia ikiwa na Alama 3 Kwa kutoa Sare michezo yote ya Nyumbani na kupigwa michezo yote miwili ya Ugenini.
Al Ahly Ndiyo timu Pekee ambayo imefuzu makundi Kwenye kundi hili Wakiwa kinala wa Kundi hili Wakiwa na Alama 9 Hadi sasa.
