December 31, 2025

Tanzania Washindwe Wenyewe Kila Goli Wakiifunga Tunisia Milioni 200

0
20251219161110_658728719_801103103610405572_640_385_85_webp.webp

Wachezaji wa Taifa Stars wameahidiwa Sh200 milioni kwa kila goli watakalofunga katika mechi dhidi ya Tunisia itakayochezwa kesho Jumanne, Desemba 30.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda, alipokutana na kuzungumza na wachezaji wa Taifa Stars waliopo Morocco, leo Jumatatu Disemba 29, 2025 ambako timu hiyo imeweka kambi kuelekea mechi hiyo muhimu.

Makonda amewahakikishia wachezaji kuwa serikali iko nyuma yao na itahakikisha motisha hiyo inalipwa kama ilivyoahidiwa. Aidha, amethibitisha kuwa tayari ametimiza ahadi ya Sh100 milioni aliyotoa kwa wachezaji baada ya mechi dhidi ya Uganda.

Hatua hiyo inalenga kuongeza morali na hamasa kwa wachezaji ili kupambana kwa nguvu zote dhidi ya Tunisia na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *