Paul Makonda ‘Watanzania Kununua Goli Kwa Shilingi Milioni 100 Taifa Stars Vs Uganda Leo’

Kuelekea mechi kati ya Timu ya ya Taifa ya wanaume (Taifa Stars), Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amesema amepigiwa simu na Watanzania mbalimbali ambao wameahidi kutoa Shilingi milioni 100 kwa kila goli watakalofunga dhidi ya Uganda Desemba 27 na ile ya Tunisia Desemba 30 na Shilingi milioni 300 endapo wataibuka na alama tatu katika kila mchezo katika mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Moroco.
Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wachezaji na benchi la ufundi la Stars kuelekea mchezo wao dhidi ya Uganda utakaochezwa Desemba 27, 2025.
“Kuwathibitisha kuwa Watanzania wako pamoja na nyinyi, juzi na jana nimepokea simu za Watanzania ninaowaamini na kuwaheshimu wameniambia nenda kawaambia vijana wa Taifa Stars tupo nao na kuanzia mechi ya Uganda na Tunisia Watanzania wananunua goli moja Sh100 milioni,” amesema Makonda.
Taifa Stars inakutana na Uganda na Tunisia, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria kwa bao 2-1 mchezo uliocheza Desemba 23, 2025.
