Rais Tshisekedi Atoa Ujumbe Mzito Ka Timu ya Taifa ya DRC Congo Kuelekea AFCON 2025
Siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yaliyopangwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 23, 2026, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, alituma ujumbe wa kutia moyo timu ya taifa na kuwa wazalendo kwa nchi.
Katika ujumbe wake kwa timu ya Taifa ya soka ya Wanaume, Rais Tshisekedi alisisitiza kuwa Serikali na watu wote wa Congo wanasimama nyuma ya timu yao ya Taifa.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mabingwa mara mbili wa Afrika (1968 na 1974), inapania kutwaa tena kombe hilo mwaka huu ikiwa na kikosi imara.
Katika miaka ya hivi karibuni, Leopards wamepitia hali ya juu na chini, lakini kufuzu kwao kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kunaonekana kama fursa ya kurejesha heshima ya soka ya Congo.
Kocha wao, Sébastien Desabre, ametekeleza programu kali, ikiwa ni pamoja na kambi ya mazoezi nchini Uhispania, ili kuitayarisha timu katika hali bora zaidi.
Huku michuano ya AFCON ya 2025 ikielekea kuwa kinyang’anyiro kigumu, kinachoshirikisha wapinzani wakubwa kama Senegal, Morocco na Nigeria, Congo inayofahamika kama ‘Leopards’ wametakiwa kupitia usaidizi huu kutoka kwa Mkuu wa nchi ya Congo, kuandika sura mpya katika historia yao
