December 13, 2025

Ahmed Ally Kazi Anayo, Achukua Jukumu la Kuwatuliza Mashabiki wa Simba

0
images-86.jpeg

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba ameandika ujumbe wa kuwatuliza mashabiki wa timu yake ikiwa ni baada ya siku ya jana baadhi yao kutangaza watakuwa na dua maalum ya kuwaombea wanaoikwamisha Simba.

Ahmed Ally ameandika ujumbe akiweka wazi kuwa wenye jukumu la kuilinda Simba ni Wanasimba wenyewe na kabla ya kuzungumza chochote fikiria kwanza maneno yako yanalinda taswira ya klabu hiyo.

“Kila mwenye damu ya Simba na amekula kiapo cha kuipenda hana budi kuilinda na kuitetea kwa gharama yeyote ile”

“Kila mtu anapaswa kutanguliza maslahi ya Simba mbele kwani sote tutapita lakini Simba itabaki hivyo ni vema tukaicha Simba kwenye ubora wa juu ili vizazi vijavyo waje kunufaika na Simba yao kama sisi tulivyonufaika kutoka kwa watangulizi wetu”

“Kabla ya kuzungumza au kufanya chochote fikiria kwanza maamuzi au maneno yako yanalinda taswira ya klabu yetu au ni kinyume chake??”

“Ni jukumu letu kuilinda Simba yetu”Ameandika Ahmed Ally

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *