Yanga Yapewa Mapumziko, Wachezaji Kurudi Desemba 15

UONGOZI wa Yanga SC umebainisha kuwa wachezaji wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves kwa sasa wapo mapumziko.
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amebainisha kuwa maamuzi hayo yametoka kwenye benchi la ufundi hivyo wachezaji watakuwa kwenye familia zao na wengine watakuwa kwenye majukumu ya timu za taifa.
Mchezo wa mwisho Yanga SC kucheza Desemba 2025 ilikuwa dhidi ya Coastal Union wakipata ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Prince Dube.
Kamwe amesema: “Benchi letu la ufundi limetangaza mapumziko kuanzia tarehe 7 Desemba mpaka tarehe 15 Desemba, wakirejea tarehe 15 watafanya mazoezi mpaka tarehe 20 Desemba kisha watapumzika tena mpaka tarehe 28 Desemba.
“Wachezaji watapata fursa ya kwenda kusherehekea sikukuu na familia zao, kabla ya kurejea tena mazoezini tarehe 29 kwa ajili ya maandalizi na wote tunafahamu kuwa mwezi Januari tuna mechi za kimataifa pamoja na za nyumbani kwa kutegemea ratiba ya bodi ya ligi itakavyopangwa,”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
