Vitalis Mayanga Afungiwa Mechi Tano na Kutozwa Faini
Mshambuliaji wa Mbeya City, Vitalis Mayanga, amefungiwa kucheza mechi tano na pia kutozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la kumpiga kiwiko kwa makusudi beki wa kushoto wa Simba SC, Anthony Mligo.
Uamuzi huu umetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) katika taarifa yao iliyotolewa leo, Desemba 8, 2025.
Kamati imeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuhakikisha usalama na nidhamu kwenye ligi, huku ikisisitiza kuwa vitendo vya ukatili ndani ya dimba havitavumiliwa. Mbeya City sasa inakabiliwa na changamoto kubwa kwani mshambuliaji wake nyota atakosa mechi kadhaa muhimu za ligi.
