Matola Anapaswa Kuwa Kocha Mkuu Simba

Dunia ya leo klabu nyingi kubwa zimekuwa zikiwapa nafasi wachezaji wao wa zamani kwa kustahili, si kwa sababu tu waliwahi kuvaa jezi za timu hizo. Ndiyo maana klabu kama Al Ahly tunaona nafasi muhimu, ikiwemo ile ya Mwenyekiti, ikishikiliwa na gwiji wao wa zamani. Hali hiyo hiyo ipo Bayern Munich, ambako utamaduni wa kuwaamini na kuwaendeleza wachezaji wa zamani umejengeka kwa muda mrefu.
Hapa nyumbani, Seleman Matola ni gwiji halisi wa klabu. Amefanya makubwa akiwa mchezaji, ameshinda mataji, na kama kocha msaidizi amefika hadi fainali ya CAF Confederation Cup.
Katika misimu kadhaa, kila anapopewa timu kwa muda, ameonekana kufanya vizuri. Haipaswi kuwa dhambi kumpa nafasi ya kuwa Kocha Mkuu. Anaijua klabu, historia yake, mila na tamaduni zake. Amewahi kufanya kazi na makocha mbalimbali, jambo ambalo linamuongezea uzoefu mkubwa wa kuiongoza klabu hii kubwa nchini.
Zaidi ya hapo, kwa mara ya kwanza katika historia ya soka letu, tumefuzu AFCON 2025 tukiwa chini ya makocha wazawa. Basi kwa nini Matola asipewe nafasi?
Imeandikwa na @mohusein_15
