December 5, 2025

Kocha Seleman Matola Apewe Simba Kuwa Kocha Mkuu, Simba Wamuamini

0
images-2025-12-05T100931.359.jpeg

Kocha Seleman Matola Kila akibakia na Timu pekee yake basi Simba lazima icheze vizuri na ushindi mnono unapatikana.

Seleman vs Fountain Gate Simba alishinda bao 3 kwa bila na mpira mwingi ulipigwa.

Seleman Vs Namungo Fc Simba ilishinda bao 3 na Mpira mwingi ukapigwa pira sasampa.

Seleman Vs Mbeya City Simba imeshinda bao 3 kwa bila na mpira mwingi umepigwa Tena hajawahi kuruhusu bao hata Moja kwenye mechi zote ambazo yeye alibakia na Timu

Sasa tunahangaika na nini kuleta wazungu kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa na wakati mzungu mweusi tunaye kwenye Benchi SELEMAN MATOLA VERON @seleman_matola ?

Ni wakati sasa wa uongozi wa Simba kufanya maamuzi magumu ya kumuamini Legendary MATOLA kwa kumkabidhi Timu kama kocha mkuu na kumpatia sapoti na ushirikiano mkubwa kama ambao huwa wanatoa kwa makocha wa kigeni Ili aweze kutekeleza majukumu yake na kuivusha Simba hapa ilipo kwenda kwenye nchi ya ahadi.

Wana Simba wenzangu naombeni tuamini makocha wazawa tuanze na MATOLA tuache maisha ya kukariri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *