December 3, 2025

Timu ya Simba Wamfuta Kazi Kocha Dimitar Pantev na Wasaidizi Wake

0
WhatsApp-Image-2025-10-04-at-09.26.38-e1759654665266.jpeg

Wekundu wa Msimbazi Simba SC baada ya kupoteza michezo miwili ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico ya Angola na Stade Malien ya Mali, wamefuta kazi Meneja wao Mkuu Dimitar Pantev.

Simba SC wamemfuta kazi Dimitar Pantev na Wasaidizi wake na sasa Seleman Matola atasalia na kikosi hadi watakapotangaza Kocha mpya.

Pantev Raia wa Bulgaria alijiunga na Simba SC October 3 2025 akitokea Gaborone United ya Botswana, amedumu Simba SC kwa siku 61, ameiongoza Simba SC kwenye mechi 5, akishinda mbili, sare moja na kupoteza mbili.

Nsingizini 0-3 Simba SC
Simba 0-0 Nsingizini
JKT 1-2 SimbaSC
Simba 0-1 Petro
Stade Malien 2-1 Simba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *