Simba Yachapika Tena Ligi ya Mabingwa

Anaandika @kelvinrabson_
✍🏼 Stade Malien walikuwa vizuri sana wakiwa na mpira na bila mpira , walikabiliana vizuri na Simba na kutumia udhaifu wao . Ubora wa Simba ni kucheza kupitia ndani kwenye kiungo : wanakuwa na Back 3 nyuma then mstari wa wachezaji wanne mbele na udhaifu wao bila mpira wanachelewa kuzuia nafasi kwenye phase zote .
✍🏼 Stade Malien wakiwa wanashambulia wanaufanya mpira utembee haraka kwenye nafasi na walitumia zaidi mawinga wao ambao wanashambulia vizuri nafasi nyuma ya Fullbacks wa Simba huku wakitengenza 1 vs 1 na CBs wa Simba ni wao wenyewe watakuwa wakatili kiasi gani , kuna mda walikosa usahihi wa pasi zao za mwisho .
✍🏼 Bila mpira Stade Malien walihakikisha wanashinda mipambano yao vizuri ( walikuwa imara zaidi ya Simba kwenye mipira ya juu na kuokota mipira ya pili ) , wanafika kwenye matukio kwa wakati sahihi na wanakuwa na idadi nzuri ya wachezaji na muundo wa 4-4-2 dhumuni kuwanyima Simba njia ya kupitia ndani .
✍🏼 Nafikiri kocha wa Simba anashindwa kudefine “ Role “ ya wachezaji wake vizuri kuanza na Maema kwenye namba 8 haikutoa nafasi nzuri kwa Simba kuzuia bila mpira na alichelewa kwenye matukio na Malien wakawa wanapata nafasi kwenye mpira na nyuma ya kiungo cha Simba .
✍🏼 Kipindi cha pili , Simba waliboresha baadhi ya maeneo kiwanjani . Kwenye kiungo wanakuwa na idadi nzuri ya wachezaji dhumuni ni kuhakikisha bila mpira wanakabiliana vizuri na Malien pia walikuwa na machaguo mengi eneo la mbele hasa wakivuka mstari wa kati tofauti na kipindi cha kwanza .
NOTE :
1: Coulibaly kacheza game bora sana ( Ufundi , kasi na usahihi wa maamuzi yake 🔥 )
2: Nkeng ule uimara wake wa mwili 🙌 mlinzi anatakiwa awe ameshiba haswa .
3: Camara mchezaji wa Simba mwenye uhai ( Defensive 🔥 )
4: Nangu na De Reuck walipunguza sana idadi ya magoli kipindi cha kwanza ( walizuia vizuri kwenye box lao ) .
5: Kiukweli Simba washukuru kwa haya matokeo ingeweza kuwa zaidi ya 2-1 .
FT : Stade Malien 2-1 Simba Sc .
Uchambuzi by : @kelvinrabson_
