Shaffih Dauda ; Yanga ni TP Mazembe Mpya

Kabla ya klabu za Tanzania kuingia kwenye ramani za soka la Ushindani wa kiwango cha juu barani Afrika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Timu ya mfano ilikuwa ni TP Mazembe ya Congo DR .
TP Mazembe alikuwa kawaida sana kwake kuifunga timu yoyote ile Afrika , Kawaida kufika hatua za juu na hata kushinda Taji la Afrika kiasi cha kuvutia wachezaji wengi wenye uwezo kutamani kuitumikia hii ni kutoka na namna walivyoijenga project yao.
Miaka imekimbia project ya Mazembe imefika ukomo na sasa Mazembe haipo tena kwenye hiyo nafasi , na sisi Tanzania kwa sasa ndio tumelishika soka la Afrika Mashariki na Kati kwenye kila kitu
Binafsi yangu Naitazama Yanga SC kama timu iliyorithi mazuri ya TP Mazembe na kuongeza mengine makubwa kiasi cha wao kwa sasa kuwa ndio timu bora ya mfano na tishio zaidi kwa ukanda wetu.
Project ya Yanga ambayo kwa sasa imefikisha miaka 4 , imeleta Fainali ya Shirikisho , Robo Fainali Klabu bingwa , Makundi Back to Back , Makombe ya Ndani back to back yaani tabia zote za TP Mazembe unazikuta Yanga SC
Kitu pekee wanachodaiwa Yanga kwa sasa ni Ubingwa wa Afrika , na kama wakienda hivi ninavyowatazama basi miaka sio mingi wanaweza kufanikiwa kushinda Taji hilo
Mchezo wa mpira ni mipango [ Project inayoeleweka
