Kiuhalisia Kundi la Simba ni Gumu, Swali ni Simba Anaenda Kushinda Ugenini Kwa Nani?
Kwenye mpira historia ni kitu cha muhimu lakini sio possible kitoke kila wakati . Nimeona Simba wanafananisha kundi lao la msimu huu na lile la mwaka 2023 .
Kipindi kile walipoteza mbele ya Raja AC na Horoya kwenye michezo miwili mfululizo na bado wakapita kwenye kundi Lao .
Nawakumbusha tu!. Msimu ule Simba walivuna Alama 6 kwa Vipers home and Away then mkachukua 3 nyumbani dhidi ya Horoya na mkafuzu hatua ya Robo Fainali .
Doubt ni msimu huu Simba wapo na timu ngumu kidogo !.. Esperance ambayo ni Favorite kwenye kundi hili then Stade Malien hawa majamaa wana project nzuri sana sio Vipers hawa .
Alafu kuna Petro Atletico msimu huu wamerejea kwenye form yao : Hawa majamaa wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kupita hatua hii + Esperance then kubwa ni Simba kupoteza nyumbani mchezo wa kwanza .
Swali ni Simba anaenda kushinda ugenini kwa nani ? 🤔 Esperance ? Ambaye kadodosha alama 2 nyumbani ? Au Stade Malien aliyemkazia Esperance 😎
Anyway Lunyasi ajipange haswa !.
