Yanga Walivyoifunga Rabat, Goli Alilolifunga Dube Leo Alilihitaji Sana
✍🏼 Yanga walikuwa timu bora kiwanjani sio kwenye kumiliki mchezo tu lakini pia walitengeneza nafasi vizuri eneo la mbele walifanya kwa ubora .
1: Yanga walitengeneza combination nzuri pembeni ya kiwanja . KULIA : wanakuwa na Mwenda , Muda na Ecua ambao walitoa msingi sahihi kwa Yanga kuifungua block ya Rabat na walibadilishana nafasi vizuri sana . KUSHOTO : kuna Zimbwe , Pacome na Maxi ambao walifanya rotation nzuri wakati wanashambulia na kuufanya uwanja uwe mpana, wanapata machaguo mengi mazuri kwasababu wapo karibu karibu sana then wakipoteza mpira wanaweka presha kwa haraka na wanakuwa karibu rahisi kurejesha umiliki wa mpira .
2: Baada ya hapo wanakuwa na idadi nzuri ya wachezaji kwenye kiungo na pembeni ya kiwanja ( create overload ) , faida yake walishinda mipira mingi ya 50/50 then waliunganisha pass zao vizuri kufika eneo la mwisho tatizo likawa kwenye matumizi ya nafasi ( Ufanisi mdogo kwenye nafasi zao )
3: Yanga bila mpira wanakuwa na muundo wa 4-4-2 / 4-1-4-1 ( Mudathir na Dube ) walikabiliana vizuri na CBs wa Rabat wakati wanaanza mashambulizi nyuma na kuwalazimisha kutumia mipira mirefu na kuharakisha kwenye maamuzi yao , faida kwa Yanga kurejesha mpira kwenye umiliki wao kwa haraka .
✍🏼 Nafikiri mikakati ya Rabat kwenye kushambulia kwa kushtukiza ( Transition ) haikufanikiwa : kwasababu ya idadi ya wachezaji eneo la mbele haikuwa kubwa ngumu kwao kushinda mipambano yao , mipira ya pili na pia walikosa machaguo ya pasi wakivuka mstari wa kati .
NOTE :
1: Pacome anafanya vitu vinatokea kwa urahisi ( QUALITY 🔥 ) : runs , ufundi akiwa na mpira mguuni , control yake + utayari kwenye kila move .
2: Mudathir , Maxi na Abuya kwenye kiungo ( walifanya kila kitu kwa usahihi : bila mpira na wakiwa na mpira )
3: Diarra kafanya kazi nzuri sana .
4: Dube alihitaji sana hili goli 🔥
5: Job na Bacca wamezima vizuri sana kwenye mkoba ✅
6: Golikipa wa Rabat “Ahmed Reda” kafanya saves nyingi nzuri .
FT : Yanga Sc 1-0 AS Rabat .
By Kelvin Rabson
