Kocha wa Simba wa Zamani Benchikha Aionya Yanga Ligi ya Mabingwa
Kocha wa zamani Simba, Abdelhak Benchikha ameitahadharisha mapema Yanga kwamba ijiandae kukutana na ugumu katika mechi dhidi ya JS Kabylie aliyowahi kuinoa kabla ya kuachana nayo mwaka huu, akisema jamaa ni wagumu mno.
“Nitaitaja timu ninayoifahamu katika kundi walilopo, yaani JS Kabylie niliyowahi kuifundisha, kiukweli kwa sasa imebadilika baada ya kumaliza matatizo ya kifedha, imesajili wachezaji wazuri,” alisema Benchikha na kuongeza;
“Naiona Yanga kama imepepesuka kiubora na kama wanataka kufanya vizuri wanatakiwa kwanza kufanya vyema kwa mechi hiyo ya kwanza nyumbani ili wasiwe na presha kubwa itakapoenda ugenini kwa pambano la pili la kundi hilo. Changamoto kubwa ya mechi kubwa kama hizo ni kila timu inataka kufanya vizuri, kwa hiyo lazima kazi iwe ngumu kwa pande zote.” Alisema Kocha huyo
