November 17, 2025

Mmesikia Huko? Mashabiki wa Simba Wamgomea Kiongozi Kuingia Bure Kwa Mkapa

0
images-76.jpeg

MMESIKIA HUKO?

Mashabiki na Wanachama wa Klabu ya Simba wamegomea ofa ya kuingia bure kwenye mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Petro De Luanda utakaopigwa Novemba 22,2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Walisikika wakisema “hatutaki bure”baada ya Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba Sc ambaye alitamka hadharani ya kwamba”kwa kuzingatia umuhimu wa mchezo uongozi umeamua kuruhusu mashabiki kuingia bure kwa Mkapa”ndipo ambapo kikundi cha mashabiki kilichokuwepo kwenye mkutano wa Ahmed Ally na mashabiki kwenye kuisukuma hamasa kuelekea mchezo huo walipolipuka wakigomea ofa hiyo.

Unahisi wangekua washabiki wa timu ya Mongolia wangeipokeaje ofa hii?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *