November 17, 2025

Mchezaji George Mpole Aibu na Kusema Alipopotelea Kimpira

0
images-75.jpeg

Nyotq wa zamani wa Geita Gold na Pamba Jiji aliyewahi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, George Mpole amezungumzia ukimya wa muda mrefu alionao kwa kufichua alikuwa akifanya majaribio na klabu ya Siwelele F.C iliyopo Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Mpole alisema majaribio hayo yalikuwa ya takriban wiki tatu wakati ligi ya nchi hiyo ikiwa inaendelea, hivyo walitaka kuwaangalia wachezaji watakaowaongeza dirisha dogo la usajili na kwa sasa amesharudi nchini akisikilizia mchongo.

“Nimerejea wiki mbili zilizopita baada ya kumaliza kufanya majaribio hayo, kama watanihitaji watanipigia simu, ikishindikana nitaendelea na mambo mengine, kwa sababu dirisha dogo la usajili litakuwa limefunguliwa maeneo tofauti,” alisema Mpole na kuongeza;

“Katika majaribio hayo tulikutana wachezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali na kilichoongezeka kwangu ni kujiamini na uthubutu wa kuendelea kupambana nje ya mipaka ya Tanzania.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *