November 17, 2025

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Liverpool inamfukuzia Semenyo Bournemouth

0


Mohamed Salah anatarajiwa kuichezea timu ya taifa Misri katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Desemba na Januari, huku Liverpool ikiendelea kuhusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo, 25, ambaye nchi yake Ghana ilishindwa kufuzu. (Liverpool Echo)

Liverpool pia inapanga kuwasilisha dau la kumsajili kiungo wa kati wa AZ Alkmaar wa Uholanzi Kees Smit,19. (Habari za Soka kupitia TeamTalk)

Roma inajadiliana naklabu ya Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkataba wa mkopoJanuari Joshua Zirkzee, 24, ambao unajumuisha chaguo la kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi msimu wa joto kwa euro 35m (£31m). (Soccer News via TeamTalk)

Ikiwa azma ya Roma ya kumsajili Zirkzee haitatimia, watamgeukia mshambuliaji wa Tottenham Mfaransa Mathys Tel, 20. (Metro)


Mshambulizi wa Chelsea na Senegal Nicolas Jackson, 24, hana nia ya kukatiza uhamisho wake wa mkopo wa msimu mzima kwenda Bayern Munich ili kukamilisha uhamisho wa kudumu katika klabu nyingine mwezi Januari. (Florian Plettenberg)

Real Madrid iko tayari kupokea ofa ya hadi euro 20m (£17.69m) – kutoka Sunderland, Aston Villa na Wolves kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa Uhispania Gonzalo Garcia, 21. (Fichajes)

Real Madrid hawana haraka ya kufanya mazungumzo ya kandarasi na beki wa kati wa Austria David Alaba, 33, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na japo hajacheza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo tangu alipouguza jeraha baya la goti Desemba 2023. (AS).

Maelezo ya picha,Mshambulizi wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal Nicolas Jackson
Mkufunzi wa United Ruben Amorim anataka kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Carlos Baleba, 21, kutoka Brighton katika juhudi za kuimarisha safu ya kati, (Mirror)
Meneja wa Rangers Danny Rohl huenda akasita kumsajili kiungo wa kati Nicolas Raskin, 24, mwezi Januari, huku Tottenham ikiwa moja ya klabu zinazoripotiwa kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Football Insider)

Tottenham inakabiliwa na tishio la kumkosa mshambuliaji wa zamani wa Everton Ademola Lookman, 28, baada ya Atalanta kubadili mameneja. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria alikosana na bosi wake wa zamano Ivan Juric kabla ya kutimuliwa. (TeamTalk)

Kiungo wa kati wa Marekani Christian Pulisic, 27, anataka kusubiri AC Milan kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao kabla ya kusaini mkataba mpya na wababe hao wa Serie A. (Calciomercato)

Manchester City inamfuatilia beki wa Eintracht Frankfurt Nathaniel Brown, 22, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza katika timu ya taifa ya Ujerumani mwezi Oktoba. (Bild – kwa Kijerumani)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *