Nahodha wa Simba Sc, Shomari Kapombe ameondolewa kwenye kinyang’anyiro cha wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Klabu za Afrika wa mwaka 2025 huku Fiston Kalala Mayele akiendelea kusalia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mayele anayechezea Pyramids ya Misri ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo sambamba na
Mohamed Chibi pia wa Pyramids na Oussama Lamlioui wa RS Berkane.
Mbali na Kapombe nyota wengine walioondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho ni Ismail Belkacem, Blati Toure, Issoufou Dayo, Emam Ashour, Ibrahim Adel na Mohamed Hrimat.
