Uchambuzi Yaliyojiri Mechi ya Simba na JKT Tanzania

Anaandika @kelvinrabson_

✍🏼 Mchezo ulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu , kasi na mabadiliko ya muundo wa uchezaji hasa kwa Simba wakati wanaanza build up ….. Kivipi ?

1: Eneo la nyuma wanakuwa na Back 3 ( Naby , Rushine na Nangu ) then Kagoma anaombea mpira nyuma ya mstari wa kwanza wa JKT wakati wanaweka presha huku Maema na anasogea juu kuombea mpira nyuma ya kiungo cha JKT .

2: Kapombe na Anthony wanasogea juu kuwaruhusu wingers wao kushambulia nafasi eneo la ndani , baada ya hapo Simba wanakuwa na namba 10 watatu kama kawaida yao ( Kibu na Mutale wanashambulia “Half Spaces” then Maema nyuma ya Mukwala lakini bado haikuwafanikisha Simba kutengeneza nafasi nyingi eneo la mbele ( kwasababu ya muundo mzuri wa JKT kwenye kuzuia ) .

✍🏼 Nafikiri kocha wa JKT “Ahmed Ally” alifanya homework yake vizuri sana : alihakikisha anakuwa na wachezaji wengi kwenye eneo la kiungo , dhumuni ni kuhakikisha wanalinda vizuri defense yao ( walifika kwenye mpira kwa wakati sahihi , shinda mipambano yao then walikuwa na muundo mzuri wa kuzuia ) pia waliweza kuunganisha pasi zao vizuri kutokea nyuma , tatizo ni wakivuka mstari kati wanakuwa na idadi ndogo ya wachezaji .

✍🏼 Kipindi cha pili , timu zote ziliamua kufunguka JKT walitoka kwenye “Low Block” na kuzuia kwenye Midblock huku idadi ya wachezaji eneo la mbele iliongezeka , lakini baada ya kuwa na uongozi wa 1-0 walishindwa kulinda vizuri + Simba walikuwa nawachezaji wengi wanaotaka mpira kwenye nafasi kuliko mguuni rahisi kwao kuifungua defense ya JKT .

NOTE :

1: Golikipa wa JKT “Omar Gonzo” kacheza game nzuri sana 🔥

2: Wilson Nangu mtulivu sana akiwa na mpira mguuni .

3: Kante kwenye kiungo alileta utulivu na msingi sahihi wa Simba kuivuka pressing ya JKT .

4: Morice Abraham alileta uhai kwenye eneo la mbele ( nafasi zilianza kutengenezwa ✅ )

5: Ally Msengi na Nassoro walicheza game nzuri kwenye kiungo .

6: Upatikanaji wa goli la JKT , utulivu wa wote wawili Paul Peter na Edo Songo

FT : JKT Tanzania 1-2 Simba Sc

By Kelvin Rabson

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *