Stephanie Aziz Ki amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu Nchini Morocco ya Botola Pro na kuisaidia Wydad AC kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Hassania Agadir.
Kwa ushindi huo Wydad Casablanca imekwea kileleni mwa msimamo wa Botola Pro wakifikisha alama 17 baada ya mechi 7 na kuiporomosha Raja AC ya Fadlu Davids mpaka nafasi ya tatu, alama 15 baada ya mechi 7.
FT: Hassania Agadir 1-2 Wydad AC
⚽ 18′ Bakhkhach
⚽ 06′ Aziz Ki
⚽ 12′ Lorch