Dar es Salaam. Kocha wa JKT Tanzania, Ahmad Ally ndiye atamsaidia Miguel Gamondi katika benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Gamondi alitangazwa jana kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars baada ya mkataba wa Hemed Suleiman ‘Morocco’ kusitishwa.
Habari kutoka chanzo cha uhakika ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeithibitishia Mwananchi Digital kuwa Ahmad Ally ndiye atamsaidia Gamondi katika kipindi ambacho atakuwa anakaimu nafasi hiyo.
“Msaidizi wa Gamondi atakuwa ni Ahmad Ally wa JKT Tanzania. Kuna mambo yanawekwa sawa kisha itatangazwa rasmi lakini kwa muda mfupi uliopo kabla ya AFCON, mtu sahihi tumeona awe Ahmad Ally,” kilifichua chanzo hicho.
Katika msimu huu, Ahmad Ally ameiongoza JKT Tanzania katika michezo mitano ya Ligi Kuu ambapo imevuna pointi saba, ikipata ushindi mara moja na kutoka sare nne.
Katika hatua nyingine, Singida Black Stars imempongeza Miguel Gamondi kwa kuteuliwa kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars huku ikiahidi kutoa ushirikiano katika kuhakikisha anatimiza vyema majukumu yake.
“Klabu ya Singida Black Stars inapenda kutoa pongezi za dhati kwa Kocha Mkuu wetu, Miguel Ángel Gamondi, kwa kuteuliwa rasmi kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
“Uteuzi huu ni heshima kubwa kwa klabu yetu na thibitisho wa ubora, taaluma na mafanikio ambayo Kocha Gamondi ameonyesha tangu alipojiunga nasi.
“Singida BS itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kuhakikisha Kocha Miguel Gamondi analeta matokeo chanya kwa Taifa Stars, sambamba na kuendeleza falsafa ya ushindani wakati akitekeleza majukumu yake ndani ya kikosi chetu,” imesema taarifa ya Singida Black