Anaandika @kevinrabson_
โ๐ผ Yanga na muundo wao wa 4-2-3-1 bila mpira na wakati wanaanza build up yao wanakuwa na muundo wa 2-4-3-1 na walifanikiwa kuivuka pressing ya Mtibwa wakati wanazuia โฆ Kivipi ?
1: Zimbwe na Mwenda wanasogea mstari mmoja wenye Maxi na Abuya na kutengeneza wachezaji wanne . Hapo wanatoa machaguo kwa CBs wao kupasia mpira na kuivuka pressing ya Mtibwa .
2: Baada ya hapo FBs wanasogea juu kuwaruhusu wingers wao ( Chikola na Edmund ) kushambulia nafasi eneo la ndani pale wanapokuwa na mpira , dhumuni ni kutengeneza idadi nzuri ya wachezaji eneo la ndani na nafasi zinafunguka eneo la pembeni .
3: Hapo inatoa msingi sahihi kwa Yanga kufika eneo la mwisho kirahisi ni Yanga wenyewe hawakuwa na matumizi mazuri ya nafasi ( ingeweza kuwa zaidi ya 1-0 hasa kipindi cha kwanza : walipata nafasi nyingi nzuri ya kuimaliza game ) .
โ๐ผ Mtibwa Sugar kuna sababu kwanini msimu huu mpaka sasa wameruhusu magoli machache , wana muundo mzuri wa kuzuia wakiwa na wachezaji wengi eneo la nyuma , wapo organized na wanafika kwenye matukio kwa wakati sahihi , wakipoteza mpira wanafanya recovering zao vizuri sana . ( Plan ya Yanga ikawa kushoot kutokea nje ya box )
โ๐ผ Kipindi cha pili Yanga walikuwa wana move mpira haraka sana kusogea eneo la juu hasa kwenda kwa mawinga wao ambao walikuwa wanapata nafasi nzuri nyuma ya FBs wa Mtibwa Sugar tatizo likawa kuweka mpira kwenye nyavu .
NOTE :
1: Golikipa wa Mtibwa Sugar โCostaโ kafanya saves nzuri zilizowaweka Mtibwa mchezoni .
2: Mohammed Hussein โZimbwe Jrโ amehusika kwenye magoli mawili mpaka sasa NBCPL ( Kafunga goli zuri sana ๐ฅ )
3: Celestine Ecua ๐ฅ goli zuri sana .
5: Buzungu kwenye kiungo amecheza game nzuri sana ๐๐ป
FT : Yanga 2-0 Mtibwa Sugar
