Tue. Nov 4th, 2025
Zimbwe Jr Azua Gumzo Wakati Wa Utambulisho Afanya Jambo Hili Iliyowaacha Mashabiki Midomo Wazi
Zimbwe Jr

Beki wa kushoto wa Yanga SC, Mohamed Hussein “Zimbwe Jr”, amevunja ukimya kufuatia tetesi zilizosambaa mitandaoni zikidai hana furaha tangu ajiunge na Wananchi akitokea Simba SC.

“Hizi habari watu wanazitoa wapi kuwa mimi sina furaha na timu niliyopo? Wao wamekuja? Ni habari mbaya sana na za uchonganishi, mimi naziona tu huko mitandaoni. Kwanza, kwa nini watu wanisemee kuwa sina furaha? Sasa niwaambie tu, kila mtu angependa kuwa mwenye furaha kwa sehemu aliyopo, hivyo mimi nina furaha kama zote kwa mahali nilipo,” amesema Zimbwe Jr.

Akaongeza tena:

“Unajua lengo mojawapo la mwanadamu katika maisha yake hapa duniani ni kuitafuta furaha, kwamba purukushani zote hizi katika maisha zina lengo la kuisaka furaha. Kila mtu anapenda kuwa na furaha kwenye maisha yake, vyote tunavyovifanya na malengo tunayoweka, na pale tunapoyatimiza huwa tunajisikia furaha. Watu waache uzushi wao na wasiwe wasemeji wangu.”

Zimbwe Jr alijiunga na Yanga SC katika dirisha kubwa la usajili msimu huu baada ya kumaliza mkataba wake na Simba SC uhamisho uliotikisa tasnia ya soka la Tanzania.