
Kwa mujibu wa taarifa, awali kulikuwa na mpango maalum wa kuuza jezi rasmi za Simba (original jerseys) kwa njia ya ziara ya mkoa kwa mkoa mpango huu ulihusisha mashabiki wenye ushawishi (influencers) wa Simba.
Kampeni hiyo ilikuwa ifanyike katika mikoa kadhaa ya Tanzania Bara, mpango wa awali ilikuwa ianze na mikoa 5 ambayo mashabiki hao wangezunguka kuuza jezi za klabu. kila influencer alitarajiwa kulipwa Tsh 5,000,000/= kwa bajeti ya elfu 80 kwa siku. Sababu walikuwa waende kukita kambi kwenye mikoa iliyopendekezwa.
Jayrutty akalipeleka swala hili klabu (Simba) ili mpango kazi uanze, huko mambo yakabadilika.
mpango ukarudishwa mezani na utekelezaji ukawekwa chini ya uongozi wa klabu. Hatimaye, zoezi hilo la uuzaji wa jezi likakabidhiwa kwa Msemaji Ahmed Ally na timu yake ya ndani ya klabu.
Jambo hili limewakatisha tamaa baadhi ya influencers waliokuwa wamejiandaa kushiriki, hali iliyosababisha kuibuka kwa kampeni ya kidigitali yenye lengo la kumshusha taswira Ahmed Ally mitandaoni, wanasema sio mwana kawanyima kibunda.
Wana wanamkataa Semaji.