Wed. Nov 5th, 2025

Miaka miwili nyuma Pape Sakho anaitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa timu ya taifa ya Senegal ilikuwa kama ndoto na kumfanya awe mchezaji pekee ambaye anacheza ligi za ndani Afrika

‎Baada ya hapo historia mpya kwenye maisha yake ya soka ikaandikwa, Hii inaonyesha kwa namna gani ligi yetu imekuwa huku waanga wa haya mafanikio ni simba na yanga

‎Leo stori kubwa imeamia kwa Pacome ZouZoua na yeye anafanikiwa kuitwa kwenye kikao cha Côte d’Ivoire akiwa ni mchezaji pekee anaye cheza ligi za ndani Afrika

‎Hii ni thamani kubwa ambayo amepewa na Yangasc na kumfanya aaminike kwa kiwango cha juu na taifa kubwa la kimpira

‎Sio kwa hao tu hata kwa misimu ambayo Mayele na Inonga wapo hapa nchini ndiyo wachezaji pekee ambao walikuwa wakiitwa kwenye kikosi cha Dr Congo ambao wanacheza kwenye ligi ndani ya bara la Afrika

‎Simba na yanga ni zaidi ya klabu zinaweza kukufanya uwe mkubwa ndani ya muda mchache lakini pia zinaweza kuharibu maisha yako ya soka ndani ya muda mfupi.