
Nchini Zambia, Serikali imesitisha msaada wake wa kifedha kwa timu ya taifa. Uamuzi huu unakuja hasa baada ya Chipolopolo kupata kichapo nyumbani cha bao 1-0 dhidi ya Niger.
Katika barua iliyotumwa kwa chama cha soka cha Zambia (FAZ), Wizara ya Michezo inataka maelezo kuhusu usimamizi wa timu na ufundishaji wa kocha Avram Grant.
Chama cha soka cha Zambia (FAZ) kina siku saba za kujibu.
Serikali inaeleza kwamba ilikuwa inalipia sehemu kubwa ya gharama za timu ya taifa kama mshahara wa kocha mkuu, bonasi, usafiri na malazi.
Hata hivyo, kutokana na matokeo duni, maafisa sasa wanataka kujua ni kwa nini fedha hizo zinapaswa kuendelea kutolewa.
Wakati wakisubiri majibu ya FAZ, ufadhili wa timu ya taifa umesitishwa.