
Unaweza ukagundua sura ya wanaume kwenye hii picha ? Hiki ndicho kitu ambacho Iran walikuwa wanatuhumiwa nacho.
Imepita miaka 10 tangu Iran walipotuhumiwa kuwachezesha wachezaji wa kiume kwenye timu ya taifa ya wanawake.
Ilikuwa story kubwa na ya kushangaza, shirikisho la soka nchini Iran lilipokea lawama nyingi kutokana na tuhuma hizo.
Ilidaiwa kwamba wachezaji nane wa timu ya taifa ya wanawake ya Iran ni wanaume waliokuwa wanashirikufanyiwa upasuaji wa kubadili jinsia.
Shirikisho la soka la nchi hiyo lilituhumiwa kwa kukosa maadili kwa kuruhusu kwa makusudi wanaume nane kuchezea timu ya wanawake.
Afisa mmoja aliyekuwa karibu na ligi ya Iran, aliiambia tovuti moja ya habari nchini humo kuwa “[Wachezaji nane] walikuwa wakicheza kwenye timu ya wanawake ya Iran bila kukamilisha upasuaji wa kubadili jinsia.”
mamlaka ziliamuru kufanyika kwa vipimo vya kubaini jinsia kwa wachezaji wote wa timu ya taifa na wale wa ligi kuu. Majina ya wachezaji waliokuwa wanashukiwa kuwa wanaume hayakufichuliwa.
Timu ya wanawake ya Iran hucheza wakiwa wamevaa hijabu, mashati ya mikono mirefu, na suruali ndefu za michezo.
Mwaka 2014, shirikisho la soka la nchi hiyo lilianzisha ukaguzi wa nasibu baada ya kugundulika kwamba wachezaji wanne wa timu ya taifa walikuwa aidha wanaume ambao hawajakamilisha upasuaji wa kubadili jinsia, au walikuwa na matatizo ya kimaumbile ya maendeleo ya kijinsia.
Mwaka 2010, kulikuwa na mashaka kuhusu jinsia ya golikipa wa timu hiyo.
Upasuaji wa kubadili jinsia ni halali nchini Iran kwa mujibu wa sheria— au tamko la kidini — lililotolewa na marehemu Khomeini, kiongozi wa kiroho wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.
Sheria hiyo inakinzana na kanuni kali za maadili ya kijinsia chini ya sheria za Kiislamu (Sharia) nchini humo, ambazo zinakataza ushoga na ngono kabla ya ndoa.
Upasuaji wa kubadili jinsia kwa kawaida hufanyika kwa hatua nchini Iran, ambapo mchakato mzima unaweza kuchukua hadi miaka miwili na unahusisha tiba ya homoni kabla ya mabadiliko kamili ya jinsia kukamilika