
Baada ya Kocha Nasserdin Nabi kuiacha kwenye mataa Klabu ya Kaizer Chiefs mawiki kadhaa nyuma Klabu hiyo bado inaonekana kusua sua kupata matokeo mazuri ikiwa chini ya waliokuwa wasaidizi wake ambao ni Cedrick Kaze pamoja na Khalil Ben Youssef.
Tangu Nabi awaachie mikoba wawili hawa wameiongoza Kaizer Chiefs katika michezo Mitano na katika hiyo wamefungwa michezo 2, Suluhu 2 na Ushindi 1.
Moja ya mashabiki wa klabu hiyo mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika mitandao ya kijamii @chrisexcel_102 kupitia ukurasa wake wa X.COM ameandika ‘Hawa matapeli wawili hajashinda mchezo wowote wa maana tangu wamsaliti Kocha Nasserdin Nabi’ akionesha hisia zake juu ya Khalil na Kaze.
Kaizer Chiefs kwasasa ipo nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini #PSL wakiwa na alama 15 walizozipata katika michezo 8 waliyoicheza.