
Kwa sasa kila mchezaji wa Yanga anaonekana wa kawaida sana. Hii inatokana na jinsi timu inavyocheza kwa sasa — haichezi kama timu na hakuna mfumo unaowawezesha wachezaji kuonyesha ubora wao binafsi.
Mfano ni jana ambapo Boyeli alikuwa anatumiwa mipira mirefu huku akiwa peke yake mbele dhidi ya walinzi wanne. Katika mazingira kama hayo, tunaweza kutarajia afanye miujiza gani? Ukweli ni kwamba kocha ana jukumu kubwa la kutengeneza mazingira bora kwa wachezaji wake ili waweze kukabiliana ipasavyo na wapinzani.
Chini ya Folz, hata Pacome kafanya nini cha ajabu? Even him mazingira ya sasa yanampa tabu. So na yeye tungekua hatumjui tengesema na yeye ni machachari tuu
Ni rahisi sana sasa kusema Boyeli, Ecua, Kouma na Chikola “hawana kitu,” lakini chanzo ni mfumo wa timu. Kocha lazima atengeneze system bora ya timu kucheza pamoja uwanjani.
Baada ya hapo ndipo tutaweza kuona nani ni machachari kweli na nani ni hatari. Kwa sasa, hata wale hatari wanaonekana wa kawaida tu. 🙌🏼