Tue. Nov 4th, 2025

Afisa Habari wa Simba SCc, amesema kwamba mchezo wa klabu hiyo Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Jumapili dhidi ya Gaborone United hautakuwa na mashabiki ndani ya uwanja, hatua iliyowekwa kufuatia adhabu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Ahmed Ally amesema kuwa adhabu hiyo ni matokeo ya mechi ya Simba SC dhidi ya Al Masry, ambapo baadhi ya mashabiki waliingia ndani ya uwanja wa kuchezea na wengine waliwasha moto. “Kilichosababisha ni mchezo ni dhidi ya Al Masry. Adhabu hii inakwenda pamoja na faini ya Dola 50,000, sawa na takriban Tsh. 120 milioni,” amesema Ahmed.

Aidha katika hatua nyingne Ahmed amewaasa washabiki waachane na vitendo ambavyo vinaing’arimu klabu, “Niwaase mashabiki wenzangu wa Simba, waache vitendo vya vurugu uwanjani. Kwanza tuanze ulinzi wa wenyewe kwa wenyewe, ukiona mtu anataka kuwasha zile ‘fireworks’ mzuie, ukiona mtu anataka kuingia uwanjani tushirikiane kumzuia ikiwezekana kumtoa uwanjani. Angalia mechi kama hii tunakwendwa uwanjani bila mashabiki. Hatupo hapa kulaumiana ila kukumbushana.” Ameongeza Ahmed.

Klabu ya Simba itacheza mchezo wao wa marudiano dhidi Gaborone United katika Uwanj