Wed. Nov 5th, 2025

Kwa dakika chache alizopata Leo na Kucheza ameifanya siku yangu iishe vizuri sana wow wow wow what a player 💪👊⚽

Ana utulivu wa hali ya juu sana akiwa ana Mpira

Ana kazi sana na maamuzi ya haraka mno

Ni mzuri kwenye kupiga pasi

Ni mzuri kwenye kufanya mashambulizi na kufanya shambulizi la kushtukiza.

Ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira

Ana uwezo mkubwa sana wa kupiga chenga.

Ball fitness ✅

Ball brain 🧠✅

Ball balance ✅

Ball technical ✅

Ball control ✅

Niseme tu hii ni hazina kubwa sana tuliyonayo Wana Simba tuilinde kwa wivu mkubwa ninamtabiria makubwa sana msimu huu ndani ya Simba kama atakuwa anaaminiwa kwa kupewa nafasi Ili aweze kuonyesha ubora wake alionao

Hongera sana bwana mdogo Morice Ibrahim âš½

Bila kumvunjia heshima Rastaman Kibu Denis , naweza kusema kutoka kwake na kuingia Morice Abraham kumeziba kila lililoonekana kuwa ni pengo jioni ya leo

Kwa dakika 45 , amepoteza kujiamini kwenye pasi moja tu nayo ni ile ya kwanza wakati anaingia , baada ya hapo aka gain temper na kila tukio lililofuata alilifanya kwa usahihi wake

Anaficha mali , ananyumbulika , anaziona nafasi , anakaa kwenye maeneo sahihi ndio maana umeona zile kosa kosa pale juu

Kiwango kizuri @mo18_official kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu NBC PL , kaaminiwa amelinda uaminifu