Wed. Nov 5th, 2025

✍️ Alama tatu za kwanza kwa Lunyasi kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi , Magoli matatu + Cleansheet ndani ya dakika 90 Simba wamefanya nini ?

✍️ Simba na 4-2-3-1 wakati wanaanza build up wanakuwa na muundo wa 2-4 ( CBs wawili nyuma then Kagoma na Mzamiru mstari mmoja na FBs wao dhumuni ni kutengeneza muundo mzuri wa kuivuka pressing ya Fountain ambayo ilikuwa na muundo wa 4-4-2 walifanikiwa kuivuka tena kiurahisi ….. baada ya hapo ?

✍️ Nafikiri ni Simba wenyewe watatumiaje nafasi wanayopata nyuma ya kiungo cha Fountain Gate maana walikuwa na idadi nzuri ya wachezaji wakivuka mstari wa kati ( wachezaji sita mpaka saba : Mzamiru , Mpanzu , Ahoua , Kibu , Sowah + FBs ) baada ya hapo tatizo likawa ni :

A) Maamuzi yao ya mwisho hayakuwa sahihi ( Walipoteza mpira kirahisi , hakuna mchezaji mwenye uthubutu wa kupiga Foward Passes kuipita kiungo cha Fountain ambacho kiliacha nafasi kubwa kati yao na walinzi + Pass nyingi zilipotea )

B) Bila mpira Simba wanaonekana kuwa wazi sana kwenye eneo la kiungo ( idadi ndogo ya wachezaji wakati wanazuia + Fountain waliivuka pressing yao vizuri na kufika eneo la mwisho tatizo kwao ni idadi ndogo ya wachezaji , maamuzi yao ya mwisho na usahihi wa pasi zao ) .

✍️ Simba kipindi cha pili walihitaji wachezaji ambao ni wazuri wakiwa na mpira mguuni na wenye uwezo wa kufanya vitu vitoke kwa urahisi ( Morice & Maema ) ambao walinufaika vizuri na nafasi nyuma ya kiungo cha Fountain “Between the lines” na nafasi kwenye half spaces lakini bado walishindwa kutoa adhabu stahiki ingeweza kuwa zaidi ya 3-0 .

NOTE :

1: KULANDANA kacheza vizuri sana kwenye kiungo 👏 kashinda duels zake vizuri na utulivu akiwa na mpira .

2: Jean Charles Ahoua ameanza mapema kuweka numbers zake vizuri ( Goal & Assist 🔥 ) .

3: Rushine De Reuck zile Foward passes zake 🙌

4: Morice Abraham ✅ Jonathan Sowah amefungua Account ya magoli 👏

5: Makosa Binafsi yamewagharimu Fountain .

FT: Simba SC 3-0 Fountain Gate

By Kelvin Rabson