
Huyo ni Ousmane Dembele anaongea na Dunia baada ya kushinda Tuzo ya Ballon d’Or
Si unamuona anatoa machozi , unajua kwanini analia .?
Stori ya safari yako inaweza kubadilika kwa msimu mmoja tu kama utaamua kuwa kama Dembele niamini mimi
machozi ya Dembele yanaletwa na yale mapito magumu aliyoyapitia kama kijana mpambanaji kwenye mpira wa miguu.
Kwa kipindi kirefu amekuwa akisumbuliwa na majeraha lakini msimu wa 2024/25 ulikuwa mwema kwake na kujikuta msimu mzima akiwa fit na injury ndogo ndogo , ndani ya msimu huo amefanya makubwa kuionesha Dunia kipi kipo ndani yake
Luis Enrique kama Kiongozi wa timu akamwambia kwa sasa hapa PSG wewe ndiye Star wetu , tumekuamini usituangushe
Dembele amemaliza msimu na magoli 35, Assists 16 kwenye mechi 53 na kuifanya PSG kutawala kila mashindano
Uwezo mkubwa alionao , kasi yake mchezoni vilifanya kila aliyemkatia tamaa ashangae kutoka kupambana na Injury hadi kuwa mchezaji bora wa Dunia ni bonge la ushuhuda kwa vijana wapambanaji wanaopitia changamoto
Msimu mmoja tu unaweza kubadili maisha yako na kila kitu kikabadilika sio mpira tu kwenye hiko hiko unachofanya kama kazi yako ya kukuingizia kipato
Digala was here ✍️