
Klabu ya Paris Saint-German imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka 2025 kwenye hafla ya tuzo ya Ballon d’Or huko Paris huku kocha wa Timu hiyo, Luis Enrique akitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Dunia mwaka 2025.
Enrique amepata mafanikio makubwa msimu uliopita akiongoza PSG kutwaa ubingwa wa Ligue 1, taji la Klabu Bingwa Ulaya, na Uefa Supercup.