
Klabu ya Yanga Sc imepata ahueni baada ya mchezo wao wa kuwania kufuzu hatua ya makundi dhidi ya Wiliete Benguela kuelezwa kupigwa katika jiji la Luanda kati ya Septemba 19-21 kupitia barua rasmi iliyoandikwa kwa klabu hiyo badala ya mji wa Benguela, yalipo makao makuu ya klabu ya Wiliete.
Mabadiliko hayo ni ahueni kwa @yangasc ambayo itakuwa inatoka kucheza mchezo muhimu wa ngao ya Jamii dhidi ya waoinzani wao wa jadi, @simbasctanzania , kwa kuwa yatapunguza urefu wa safari.
Kwa kawauda umbali wa kutoka Jiji la Luanda hadi Benguela ni umbali wa takribani saa nane kwa basi, hivyo mchezo kufanyika Luanda itawapunguzia Yanga Sc safari ya masaa nane kwa basi na hii ni faida zaidi kwao kwa kuwapunguzia wachezaji wake uchovu