Yanga VS Bandari Leo Yanga Day Saa Ngapi?


Baada ya watani wao wa jadi, Simba SC,almaharufu kama wekundu wa msimbazi kukamilisha sherehe ya siku yao inayojulikana kama Simba Day mnamo tarehe 10 Septemba 2025 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, sasa macho ya mashabiki wa soka nchini Tanzania yanahamia kwenye tukio lingine kubwa Wiki ya Mwananchi 2025 (Yanga Day). Sherehe hii ya kipekee inatarajiwa kuufanya Uwanja wa Benjamin Mkapa kulipuka kwa shamrashamra mnamo 12 Septemba 2025, ikisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Yanga SC dhidi ya Bandari FC ya Kenya.

Saa Ngapi Mchezo Utaanza?

Swali ambalo limekuwa likiulizwa na mashabiki wengi ni: “Yanga VS Bandari 12/09/2025 Saa Ngapi?”
Kwa mujibu wa ratiba rasmi, mchezo huu utaanza saa 11:00 jioni na utarushwa mubashara kupitia Azam Sports 1 HD.