
Anaandika Micky Jnr mwandishi wa habari za michezo kutoka Nchini Ghana Kuhusu Allan Okello:
Simba SC wamekuwa wakimfuatilia muda mrefu kupitia scouting wao, lakini kwa sasa hakuna dili lolote lililo karibu kukamilika.
Klabu tayari ina viungo wengi wa namba 10 na kwa kuwa Feisal “Fei Toto” Salum yupo mbioni kutua, nafasi ya Okello haitahitajika.
Kama ilivyoripotiwa, Fei Toto amekubali kujiunga na Simba na mpango ni huu:
▫️ Kusaini mkataba wa awali Januari 1
▫️ Kamilisha usajili wake mara tu mkataba wake na Azam utakapomalizika
Huyu ndiye “X factor” ambaye Fadlu Davids amekuwa akizungumza kumhusu.