Clatous Chama
Clatous Chama

Nyota wa zamani klabu ya Simba Clatous Chama ameweka wazi kuwa amepita vilabu vingi ila Simba SC imenifanya kuwa mchezaji wa kipekee mno na kudai kuwa Msimbazi ni zaidi ya nyumbani.

“Nimepita timu tofauti tofauti, lakini Simba SC ina upekee sana, nikianza kutaja kimoja kimoja siwezi kumaliza ila imenipeleka mbali zaidi, imenifanya kuwa mchezaji wa kipekee mno, pale ni nyumbani ni familia tena inaweza kuwa zaidi, nawamisi, kila wakati watabaki moyoni, sio kwamba nilikopita hatukuishi vizuri, hakukuwa na mahusiano mazuri,ila Simba SC ni zaidi, ndani ya uwanja hadi nje.” – Chama JR

Vilabu Mbalimbali alivyotumikia Mwamba wa Lusaka

2016 – ZESCO United
2017- Al Ittihad
2017-2018 Lusaka Dynamos
2018-2021 Simba SC
2021-2022 RS Berkane
2022-2024Simba SC
2024-Young Africans
2025 – Singida BS

Ikumbukwe kuwa Chama JR alijiunga na Simba SC mnamo mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya nchini kwao Zambia na baada ya kutua Simba SC alifanya vyema zaidi na jina lake kuwa kubwa mno ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.