Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (JK), amekanusha taarifa zilizodai kuwa gari lililoanguka katika msafara wake lilikuwa gari lake binafsi, akieleza kuwa yeye hakuwepo ndani ya gari hilo.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kivule, jijini Dar es Salaam, Kikwete amesema gari lililopata ajali lilikuwa linamilikiwa na rafiki yake ambaye alikuwa akisafiri na watoto wake pamoja na dereva.

Ameongeza kuwa hakuna mtu aliyedhurika kwenye ajali hiyo, huku akifafanua kuwa chanzo cha ajali kilikuwa ni dereva kujaribu kumkwepa mtu aliyekuwa barabarani.