
Yanga wanaamini thamani ya Mzize inazidi kupanda siku hadi siku kutokana na kiwango cha Mzize kwenye michuano ya CHAN.
Kabla ya CHAN kuanza Yanga walikadiria Mzize ana thamani ya $1m ila kutokana na kiwango chake kwa siku za hivi karibuni Yanga wanahisi thamani yake imepanda zaidi na kama ataendelea kukiwasha basi thamani yake itapanda zaidi hadi $2m.
Mauzo ya wachezaji ni biashara kubwa duniani,thamani za wachezaji zinabadilika kila kukicha kutokana na viwango vyao,Yanga pia wanalijua hilo.
Mzize kwa sasa ni Lulu hivyo hauzwi kwa hasara.
“Ofa ya mwisho ya Mzize iliyokuja ni dollar million 2 [Billion 4.9 TZS], sisi kama viongozi tukamuongezea maslahi yake na sasa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi kwenye timu yetu.”
“Akimaliza msimu huu atakuwa amebakiza mkataba wa msimu mmoja, halafu biashara itafanyika.”
– Eng. Hersi Said, Rais wa klabu ya Yanga.