Wed. Nov 5th, 2025

Katika Muendelezo wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Mgombea mwenza wa Urais wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho kitaendelea kuwachukua wapinzani wenye akili ili kushirikiana nao katika kuleta maendeleo nchini.

Nchimbi ameyasema hayo leo Agosti 31, 2025 akiwa Tarime Mjini na kueleza kuwa CCM inawahitaji watu hao wenye akili “Wale wote waliopo kwenye vyama vingine ambao wana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kutafakari maendeleo tutakuwa tunawakamata mmoja mmoja na tunawaleta kwenye chama chetu washirikiane na CCM kujenga nchi”.Dkt. Nchimbi

Ameongeza akisema “Kwa mfano hamuwezi kuwa na mtu Tarime mwenye akili mwenye uwezo mkubwa mnamuacha anakaa upinzani mnasuburi nini si lazima umrudishe aendelee kujenga Chama na nchi kupitia CCM”

Akiendelea kuzungumza aliwauliza wananchi “Hizi siku za Karibuni tumemrudisha nani? Tumemrudisha nani? Tumemrudisha?” wananchi walisikika wakijibu “Matiko”.