
Ameandika Mchambuzi Scanda24 :
“Leo nimekuwekea PICHA ya Mtu anaitwa ZAMBRO kutoka Taifa la IVORY COAST, kule kwao naye mdogo kama yule Mwandishi wa Ghana lakini hapa kwetu wamepewa ukubwa ili kuzima ndoto na kuwakatisha Tamaa wa hapa kwetu. Huyu Zambro wengi mtakua mnamfahamu kwa kuwa ameleta hao wachezaji pichani, analeta wachezaji kwa vilabu vyote na bado vilabu havinuni kama wafanyavyo kwa wazawa.
.
Wakati kurasa Rasmi za klabu kubwa ziliposti muhuri wa “WINGA AMEKATALIWA” kukiwa na maboresho ya Kanuni na mambo kadhaa wa kadhaa pamoja na Wageni wengi kuwa MADALALI wa wachezaji na Sio mawakala basi vilabu vyetu vimewashikilia na kuwadharau WAZAWA, nataka sasa Tuongee Kiume, mimi nikiongea kama Mwanaume MZAWA.
.
Baada ya Wachezaji wazawa kuanza kupanda THAMANI vilabu vinataka vilete UTAPELI na kuwaita Wasimamizi MAWINGA, eti wakisema hawana LESENI, wao ni mabingwa wa kuvujisha “HIO ISAMBAE” kupitia WAJARIAMALI wa kwenye media Tanzania sasa wavujishe na hizi ya kwamba huyo anayeleta Wachezaji hana LESENI kama anayo waanze kuposti.
.
Wakati tukiwaita Wasimamizi wa ndani MAWINGA hawa wa NJE ni kina nani..? Au sababu wanatoka NJE..? Hii IDEA ya Kuwadharau wazawa inanikera mnoo, inanikera kwa sababu inaongozwa na Chuki na sio HAKI na Taratibu, ila nasema mwisho wa Utapeli unakaribia sababu tutachukua hatua za kulinda mustakabali wa UZAWA (Wachezaji na Wasimamizi)
.
MY TAKE:
Vilabu vinajichimbia Kaburi na kupandisha Gharama za wachezaji wazawa sababu ya hii michezo yao ya KIHUNI, Hawa wasimamizi wa Wachezaji nao ni WAHUNI hivyo itakua “VITA YA KIHUNI”, kule Ulaya Waliwahi kumliza hadi BABU FERGUSON na akanyimwa mchezaji na baadaye akawa anamwaga pesa. Suala la muda.
.
Wasimamizi Wazawa wanaitwa MAWINGA, Hawa Wa Kuja tuwaitaje..? Leta jina…….
.
NB:
Kwa Heri Ukoloni, Kwa Heri Uhuru (Vita Ya Kihuni)
.
PROJECT MANAGER”
Binafsi hapa sitii neno….
Wananiitaga MJUMBE, na MJUMBE hauwawi 🗣️📢