
Kuna uwezekano wa Antony Mligo,kuvunja mkataba wake na Simba.
Mligo anaidai Simba hela yake ya kusaini (Sign-on fee) Ila hadi leo anapigwa tarehe ambazo hazieleweki.
Simba walimsainisha Mligo mkataba wa miaka mitatu wakamwambia ajiunge na timu kwenye Pre-season Misri,Kisha wakamuahidi baada ya wiki mbili watamuingizia mzigo wake kwenye account.
Baada ya muda huo kupita bila chochote,kijana alikumbushia juu ya malipo Yake ila majibu aliyopewa hayarishishi,kijana alifikisha malalamiko yake kwa kocha Fadlu juu ya Jambo hilo na Fadlu akaamuru alipwe mara moja ila ikaja kubainika ndani ya Simba kuna kiongozi mmoja amegoma kusaini cheque ya malipo yake.
Ukweli ni Kwamba pesa ya kijana ipo ila inakwamishwa na kiongozi mmoja,ambae ana sababu zake Binafsi ila Fadlu anamkubali sana kijana.
Mbaya zaidi Mligo amegundua Wachezaji wote wapya wa Simba tayari wamelipwa pesa Zao za kusaini ila yeye pekee ndo bado……Hali hiyo inamuumiza kijana mpka amefikiria kuondoka.
Ujumbe wa mchambuzi wa michezo Hans rafael.
NENO MOJA KWA MSIMBAZI???
NB: UKATA SIO MZURI