
“Ni timu ninazozipenda ndio maana nimeona kitu pekee kitakachoonesha upendo ni kuchora tatoo, ambayo inawakilisha klabu ninayoitumikia na timu yangu ya taifa ya Cameroon ambao nao wanaitwa Simba wasiofungika. Najisikia faraja na naamini nitakuwa nimewajibu vyema watu ambao walikuwa wanajiuliza kuhusiana na jambo hilo” Alisema Ateba akiwa na kikosi cha Simba SC.
Kwa sasa Ateba ameuzwa uarabuni kwa Dollar $300,000 katika klabu ya Al Shorta SC ambayo ni mabingwa wa ligi hiyo msimu wa 2024/2025.